Saturday 31 May 2014

WAJAWAZITO TANZANIA WAJIFUNGULIA MALAWI

TUJIKUMBUSHE MAKALA HII NA KUTAFAKARI

*Unafuu na kutotozwa fedha wala vifaa, kivutio tosha.
Na Gordon Kalulunga.
SERA ya Afya ya mwaka 2007 haifahamiki wilayani Ileje katika mkoa wa Mbeya. Ni katika sera hii ambamo inatamkwa kwamba wajawazito nchini watapewa huduma za afya bure.

Kama sera inafahamika, basi haitekelezwi. Baadhi ya wajawazito katika wilaya ya Ileje wanaacha zahanati, vituo vya afya na hospitali wilayani mwao na kuvuka mpaka hadi nchini Malawi kufuata kinachoitwa “huduma bora.”

Kwa mfano, wajawazito kutoka kata za Bupigu, Itumba na Isongole wanafahamika kwa kwenda nchini Malawi kwa wingi ili waweze kujifungulia huko na kupata huduma nyingine za afya.

Lakini kutoka Isongole hadi hospitali maarufu ya Chitipa nchini Malawi ni umbali wa kilometa 45; wakati umbali wa kwenda hospitali ya serikali ya Ileje ni kilomita tatu tu.

Mwanamke mkazi wa kijiji cha Ikumbilo, kata ya Chitete wilayani Ileje, aliyejitambulisha kuwa anaishi na virusi vya ukimwi (VVU) anasema aliwahi kujifungulia hospitali ya Chitipa na mpaka sasa anapata matibabu yake huko.

Kuna nini katika hospitali ya Chitipa nchini Malawi hadi wajawazito wakimbilie huko? Jibu analo Neema Mbughi mkazi wa kijiji na kata ya Bupigu.

“Pale hospitali ya Chitipa hubebi chochote wakati unakwenda kujifungua. Hatuendi na madishi, karatasi za nailoni (ambako mjamzito huhala wakati wa kujifungua) wala glovu. Kila kitu ni bure, hata chakula ambacho kimepikwa kama kimetoka nyumbani,” anaeleza Neema.

Wilaya ya Ileje ina hospitali kubwa mbili – hospitali ya serikali mjini Ileje na ile ya misheni ya Isoko. Hizi ndizo hospitali ambazo zinategemewa kwa huduma ya uzazi.

Wanawake wapatao 27 waliohojiwa, pamoja na kutofautiana katika mambo mengine, wengi waliafikiana kuwa katika hospitali ya Chitipa, wauguzi wanatumia “lugha nzuri” inayompa matumaini mjamzito.

Sababu nyingine walizotaja ni kutotozwa fedha yoyote ikiwa gharama kwa kujifungulia hapo; kupewa dawa zinazohusiana na uzazi bila kulipia na kupewa chakula bure.

Hivi wanapitaje mpakani penye idara ya uhamiaji? Jibu unalopewa ni kwamba hawapiti mpakani kwenye ofisi za serikali. Wanapita vichochoroni ambako wanaita “njia za panya.”

Bali wakifika hospitalini Chitipa wanajieleza kuwa wanatoka vijiji vya ndani ya Malawi – wengine wakitaja hata ndugu zao na viongozi katika maeneo hayo kuthibitisha kuwa wanatoka humohumo.

’Neema anasema wanalazimika kusema kuwa wanatoka Malawi “…ili tuweze kupata huduma za kliniki, mahali bora na bure pa kujifungulia na matibabu mengine.”

Siyo wajawazito peke yao wanaoingia Malawi kwa matibabu. Wananchi wengine huenda hospitali za Chitipa na Kameme kupata matibabu; tena bila kutozwa fedha zozote.

Henry Kayuni, mkazi wa Bupigu anasema licha ya kufuata matibabu na mahitaji mengine kama mafuta ya taa, mbegu za mahindi, sukari na mbolea, baadhi yao wanapeleka pia watoto wao shuleni.

Anasimulia kwamba kujieleza kuwa unatoka Malawi kunasaidia “…hata kusomesha watoto nchini humo mpaka Darasa la VIII. Baada ya hapo wanakuwa tayari wamejua vema Kiingereza; ndipo wanahamishiwa Tanzania na kuwaombea nafasi Kidato cha II.”

Lida Kibona wa kijiji cha Itumba, anasema yeye alianza kupata matibabu bure katika hospitali ya Chitipa hata kabla hajapata ujauzito na kwamba manesi ya madaktari “wanasikiliza na kujali sana wagonjwa.”

Kuna kichocheo kingine kwa wananchi wa Tanzania kutibiwa Chitipa. Katika mahojiano nao Novemba mwaka jana walieleza, mmoja baada ya mwingine, kuwa ikitokea “bahati mbaya” mama au mtoto akafariki na wakati huo umejitambulisha kuwa unatoka Tanzania, basi inasafirishwa hadi mpakani bila gharama yeyote.

Katika hospitali za mkoani Mbeya karatasi la kutandika wakati wa kujifugua linauzwa kwa Sh. 3,000, paketi ya glovu Sh. 2000, beseni Sh. 3,000 na kama mjamzito amelazwa, basi hujitegemea pia kwa chakula.

Jane Kabuje mkazi wa kata ya Isongole anasema kuwa yeye ni mmoja wa wanawake wanaopata huduma za afya Chitipa nchini Malawi ingawa hospitali ya wilaya ya Ileje ipo ndani ya kata yake.  

Mkazi wa Bupigu wilayani Ileje, Amos Shimwela anasema tatizo linalowakumba wakazi wa vijiji vya mpakani hadi kuamua “kujitambulisha” kama raia wa Malawi, ni kutokana na kutopata huduma za afya nchini ambazo alisema ni ghali wakati nchini Malawi ni bure.

Naye mkazi wa kijiji cha Bulambya, Joseph Kapange anasema bora kujitambulisha kuwa ni raia wa nchi nyingine ili upate huduma, kuliko kung’ang’ania utokako ambako hupati huduma muhimu kwa afya yako.

Anasema wakati matibabu katika hospitali ya Chitipa na huduma kwa wajawazito ni bure, nchini Tanzania bado wanatozwa fedha na wengi wanashindwa hata kulipa Sh. 500 ili kupewa kadi ya kumwona daktari.

Hata wanaomudu kulipa kiasi hicho cha fedha, bado wanalazimika kununua dawa katika maduka nje ya hospitali.

Mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mama Minga, anasema baadhi ya wanaume wamekuwa wakipeleka wake zao wajawazito katika hospitali ya Chitipa miezi mitatu kabla ya kujifungua.

Amesema hii ni kwa tahadhari kwa vile wanaishi mbali na hospitali hiyo; na kwamba hawataki kusubiri hadi wajawazito wazidiwe, “…kwani usafiri wa barabara siyo wa uhakika.”

Mwandishi wa makala aya anapatikanakwa simu 0754 440749 barua pepe kalulunga2006@yahoo.com na website; kalulunga.bogspot.com

 WASOMAJI KUTOKA JF WANACHANGIA HIVI
  1. aiseee! hawajapatiwa bajaji bado? halafu hofu yangu kubwa tuna mgogoro na hawa wamalawi...
    2. Mlimpa kura Kibona, Leo yeye anawapa Chumvi na Mipira. Pole wana Kapelekesyi.
  2. Quote By zumbemkuu View Post
    aiseee! hawajapatiwa bajaji bado?
    halafu hofu yangu kubwa tuna mgogoro na hawa wamalawi...
    Mkuu CCM wanapiga sanaa hata kwenye uhai wa watu na usalama wa nchi!!
    Sijui hao wamalawi wakiamua ........!!!?

    Ukweli ni maji ya chumvi unayotakiwa kuyaoga, ukiona mahali panawasha usiyachukie hayo maji....jua hapo pana jeraha pafanyie kazi.
  3. Quote By Ruppy karenston View Post
    Aisee njia za panya kwa mama mjamzito?km 45?serious? Wanatake a very big risk. Serikali sikivu imesikia shida zao.
    Mkuu hii nchi unaweza kujilipua!!
    Hakuna anaehangaika na habari hii serikalini kama habari ya CDM kuonekana inajiimarisha vijijini! Serikali yetu imepoteza sifa kabisa!
    Ukweli ni maji ya chumvi unayotakiwa kuyaoga, ukiona mahali panawasha usiyachukie hayo maji....jua hapo pana jeraha pafanyie kazi.
  4. Nchi hii ya Malawi ni maskini zaidi kiresources ukilinganisha na Tanzania, lakini kiukweli huduma katika mahospitali na shule zake (hasa za msingi) ni bora mno ukilinganisha na huko kwetu!

  5. wajifungulie hospitali zetu hizi? Zenye huduma mbovu na vifaa haba mpaka viongozi wanakimbilia india????
    Quote By pmwasyoke View Post
    Nchi hii ya Malawi ni maskini zaidi kiresources ukilinganisha na Tanzania, lakini kiukweli huduma katika mahospitali na shule zake (hasa za msingi) ni bora mno ukilinganisha na huko kwetu!
    Then mkulu anachekacheka tu katikati ya shida kama hizi!! Mzima huyu?
    Ukweli ni maji ya chumvi unayotakiwa kuyaoga, ukiona mahali panawasha usiyachukie hayo maji....jua hapo pana jeraha pafanyie kazi.

  6. Unaweza ukajuta kuwa Mtanzania bora ukawa Mmalawi nchi maskini sana kuliko Tanzania.
  7. Quote By ANETHE
    Unaweza ukajuta kuwa Mtanzania bora ukawa Mmalawi nchi maskini sana kuliko Tanzania. 
    Cha ajabu wanasiasa wetu toka chama Tawala yaani CCM ....hawataki kabisa habari kama hizi ziongelewe....!! Mwingulu anasema simu vijijini ndio maendeleo haswa ya nchi!!
    Ukweli ni maji ya chumvi unayotakiwa kuyaoga, ukiona mahali panawasha usiyachukie hayo maji....jua hapo pana jeraha pafanyie kazi.
  8. kiukweli habari hii imenitoa moood yoote. yani mi kama Mtanzania sina cha kujivunia. udini,migomo,uzembe uliopindukia wa watumishi wa umma,rushwa na mengineyo yenye sifa za ovyo ovyo ndo sifa yetu.....ooooh God
  9. Quote By mmteule View Post
    kiukweli habari hii imenitoa moood yoote. yani mi kama Mtanzania sina cha kujivunia. udini,migomo,uzembe uliopindukia wa watumishi wa umma,rushwa na mengineyo yenye sifa za ovyo ovyo ndo sifa yetu.....ooooh God
    Pole mkuu, moyo wako wangekuwa nao kina JK nchi yetu ingepunguza aibu hizi za kijinga!
    Ukweli ni maji ya chumvi unayotakiwa kuyaoga, ukiona mahali panawasha usiyachukie hayo maji....jua hapo pana jeraha pafanyie kazi.
    Hamna shida kama madactari waliambiwa wakatafute wanapoweza kulipwa vizuri,kuwa na mazingira mazuri yaa kazi na WEWE mwananchi ukakaa kimya sasa maana ya kauli ile ya mkuu wa kaya maana yake na mwananchi kama waweza kutafuuta mahali ukahudumiwa vizuri we nenda tu..tusidanganyane jamani hakuna mfanyakazi akaambiwa kauli kama ile seuze mtu wa afya Arafu eti akamchangamkia mgonjwa kwa kauli njema na ukarimu watu wanafanya kazi aimradi mkono uende kinywani basi so kama wewe mwananchi unajiona waweza kwenda India,Agakhan,Malawi,Zambia kwa kalumanzila We nenda tu tuliokaribu na secta ya afya ndo tunawaambia hivyo otherwise kama hukumuelewa mkuu JK...akimfukuza mhudum wa afya unachekelea harafu utegemee huduma njema this is rediculous!! Wattu wapo kazin kimwili lakini kiroho wapo kunako miradi yao kuboresha maisha.....ni hayo tu.
    Reply With Quote
    Quote By prince alen View Post

    Kauli nzito hii mkuu! Like
  10. Reply With Quote
    Sielewi ni nini au kipi kinasumbua.Kwani seikali inatoa pesa nyingi sana wizara ya Afya.Ninachokiona sasa ni ma DMOs,wafamasia wilaya,maafisa Afya wakishirikiana na wahasibu na wazabuni kufisadi pesa nyingi sana zinazopelekwa mawilayani!kwani hawa serikali imeshindwa kweli kuwabana?Kama leo kwa makusudi kabisa ukianzisha uchunguzi wa kina utakuta DMOs wengi wana utajiri wa kutupa!wanafanya biashara gani ambazo wengine haziwapi utajiri huo?Ndio maana wananchi wanaona serikari imeshindwa tuu!
  11. Quote By kibaravumba View Post

    Kwahiyo serikali haijashindwa kazi?
    Quote By kibaravumba View Post
    Sielewi ni nini au kipi kinasumbua.Kwani seikali inatoa pesa nyingi sana wizara ya Afya.Ninachokiona sasa ni ma DMOs,wafamasia wilaya,maafisa Afya wakishirikiana na wahasibu na wazabuni kufisadi pesa nyingi sana zinazopelekwa mawilayani!kwani hawa serikali imeshindwa kweli kuwabana?Kama leo kwa makusudi kabisa ukianzisha uchunguzi wa kina utakuta DMOs wengi wana utajiri wa kutupa!wanafanya biashara gani ambazo wengine haziwapi utajiri huo?Ndio maana wananchi wanaona serikari imeshindwa tuu!

    mjomba temeke hospitali tu xray ya kubahatisha wanashindwa kuboresha mjini wataboresha vijijini????

    Hiyo hela wanayofikisha haitoshi hata kununua gloves itakuwa kutoa huduma bora? Kununua madawa na mengineyo?
    Hakuna cha maana zaidi ya serikali iliyojaa wanasiasa watumia tumbo.
  12. Quote By BADILI TABIA View Post
    mjomba temeke hospitali tu xray ya kubahatisha wanashindwa kuboresha mjini wataboresha vijijini????

    Hiyo hela wanayofikisha haitoshi hata kununua gloves itakuwa kutoa huduma bora? Kununua madawa na mengineyo?
    Hakuna cha maana zaidi ya serikali iliyojaa wanasiasa watumia tumbo

    Eti jamaa anasema pea mingi sana inaendas mahosipitalini! Hii kitu inabidi srikali ito majibu yenye akili!

No comments:

Post a Comment