by Gordon
Kalulunga
TANGU niwe
mmoja wa waandishi wa habari 5 waliobahatika kufauru usaili kati ya waandishi
72 Tanzania na kujifunza na kubobea kuandika habari za afya ya uzazi nchini
Tanzania tangu mwaka 2012 nimejionea, nimesikia, nimegusa, nimenusa wakati
mwingine kuyaishi maisha na wanawake wajawazito na hata ambao bado hawajawa
wajawazito.
Nieleze wazi
kuwa mafunzo hayo niliyapata kupitia program ya Fellowship inayoratibiwa na
mfuko wa vyombo vya habari Tanzania maarufu kama Tanzania Media Fund (TMF) na
kufundishwa na madaktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi.
Moja ya
mambo ambayo nilijifunza kutoka kwa wataalamu hasa madaktari nikiwa field,
kusoma mitandao na baadhi ya wanawake waliosema wazi wazi kuhusu dalili za
ujauzito na kati ya nyingi nilizoelezwa kati yake 13 nimeona nikushirikishe
katika makala hii ya uchambuzi.
Mwanamke
anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida.
Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.
Inaonesha
kuwa homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha
mabadiliko kadhaa katika mwili wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya
uchunguzi halisi wa kujua kama mjauzito au la.
1. Maumivu
kwenye matiti.
Hii ni
dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati
yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya
matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.
2. Maumivu
mwilini
Baadhi ya
wznawake wanajisikia maumivu kama vile wanataka kuingia katika siku zao. Kwa
kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha
mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha
maumivu hayo.
3. Kutokwa
damu bila kutegemea
Wanawake
wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao.
Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25
ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai na iwapo utaona hedhi inakuwa fupi au
inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, mwanamke anashauriwa kwenda
kufanya kipimo cha ujauzito au kujipima mwenyewe na kifaa cha kupimia
ujauzito..
4. Kuchoka
Mwanamke
anapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati akiwa kazini,
wakati huo mwili wake unakuwa unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha
mabadiliko.
Inaelezwa
kuwa katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza
kutumia sehemu ya nguvu za mwanamke na hivyo kumletea uchovu na usingizi.
5. Chuchu
kuwa nyeusi
Chuchu
huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza
kufanya kazi kwa nguvu zaidi hata hivyo wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi
kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.
Hali hii
huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za
asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
7. Mwili
kuvimba
Kuna wakati
kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kumsababishia mwanamke kuona
tumbo limevimba na nguo zikawa zinambana kutokana na chakula kujaa katika
utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema
ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
8. Kwenda
haja ndogo mara kwa mara
Mwanamke
kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu kimeanza kufanya kazi ya
ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa
ujauzito.
Hali hii pia
hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali
yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.
Kutokana na
mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke
kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili
wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma
alikuwa hayapendi.
10. Kuumwa
kichwa
Kuongezeka
kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika
wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha
na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.
11. Kufunga
choo.
Homoni
ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo
wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza
kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
12. Kuwa na
hasira
‘’Kutokana
na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia
uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama
wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.
Kipimo cha
joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto
huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo
ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna
“mtoto anakuja”.
0754 440749
No comments:
Post a Comment