Saturday 31 May 2014

CHAGUA JAWABU SAHIHI KWA SWALI HILI.....

JE UNA WATOTO NJE YA NDOA ULIOPATA BAADA YA KUFUNGA NDOA?

(a) Ndio na mke anajua (b) Ndio na mke hajui (c) Ndio na mume hajui

(d) Ndio mume anajua (e) Tulitoa mimba (f) Sina.


TOA MAONI YAKO KWA KUBOFYA NENO COMMENT KISHA ANDIKA JAWABU NA HATA KAMA UNA SABABU PIA....

Save the Children yatoa ripoti na wito Kukomesha vifo vya Watoto Wachanga Ulimwenguni


"Siku ya kwanza ya uhai wa mtoto ni wakati wa hatari sana na akinamama wengi hujifungua wakiwa peke yao, sakafuni majumbani mwao au hata vichakani bila msaada wowote wa kuokoa maisha. 
 
Tunapata taarifa za kutisha kuhusu akinamama kutembea umbali mrefu kwa masaa mengi huku wakiwa na uchungu, ili wapate msaada wa kitaalamu." anasema Jasmine Whit Bread, Mkuu wa shirika la Save the Children wakati wa uzinduzi wa ripoti ya hivi karibuni. 
 

JK to health workers: You can stop maternal and child deaths

President Jakaya Kikwete has appealed to health workers in the country to ensure that lives of women and children are not at risk during delivery.
Calling it a major national silent emergency, President Kikwete said it is a unacceptable that as many as 455 women out of every 100,000 live births die during delivery in a country boasting a comprehensive health system.

The president was giving his remarks during the launch of the ‘Tanzania countdown and a promise renewed on reproductive, maternal, newborn and child deaths’ in Dar es Salaam yesterday.

President Kikwete said while a lot has been achieved during the implementation of the Millenium Development Goals (MGDS) there were still sad stories of women and children who die for reasons which could be avoided.

He said the medical personnel and stakeholders must fight for increased utilisation of family planning services while also increasing the percentage of skilled health providers in the health sector.

He stated that many of the births were being conducted by traditional birth attendants who cannot handle delivery complications.

“We do not underrate the work done by these traditional birth attendants but measures must be taken to upgrade the qualifications of those dealing with helping pregnant mothers to deliver,” he said.

He asked the health ministry to make sure that men ware also included in programmes aiming to reduce maternal deaths in the country.

The president asked the health ministry to introduce Maternal, Newborn and Child Health (MNCH) scorecards in all regions in the country which will show the regional performance in dealing with maternal and child health care problems.

He said the scorecards would allow effective supervision of the activities on reproductive health activities in respective regions by health officials.
The president said he himself will want to get the regional reports every four months “and not in six months as some officials suggested.”

“Matters concerning maternal and child health are very close to my heart. I will therefore want to have these scorecards every four month to know those regions which perform well and those which underperform.

He commended Singida Region for making sure that life saving items for women and children were readily available in the region.

Tanzania is one of the ten countries contributing to 61 percent and 66 percent of the global total of maternal and newborn deaths, respectively.
According to sources maternal mortality ratios are lowest in Dar es Salaam, Arusha and Kilimanjaro regions.

Mtwara, Tabora, Tanga, Lindi and Pwani have institutional maternal mortality ratios exceeding 200 per 100,000 live births.

Meanwhile President Kikwete has observed that some of the non-governmental organisations were diverting funds meant for maternal and child health affairs.
“We have organisations, although not many, who use funds meant to help maternal and child health activities for their own benefit,” he said.

“Instead of healing many mothers and children they help their own children,” he noted. 

SOURCE: THE GUARDIAN

TACAIDS; WANAOSAMEHE HAWAPATI MAAMBUKIZI YA VVU


Afisa utafiti wa tume ya kudhibiti Ukimwi nchini(TACAIDS) Dr. Avoldia Mlokozi. 

 
Na, Gordon Kalulunga
 
TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema wanandoa na watu walio kwenye mahusiano, wakiwa na tabia ya kusameheana wanapokoseana, wanaweza kupunguza ongezeko la maambukizi ya VVU.

Hayo yalisemwa na afisa utafiti wa tume hiyo Dr. Avoldia Mlokozi alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya katika mohojiano maalum.

‘’Ukitaka kuishi kwa usalama ni kuwa na msamaha kwa mwenzako badala ya kuchepuka kwenye ndoa kwa kisingizio cha kuudhiwa na mwenza wako’’ alisema Dr. Mlokozi.

Alisema katika kanda ya nyanda za juu kusnini magharibi, kiwango cha maambukizi ya VVU, mkoa wa Mbeya una asilimia 9, Rukwa 6.2 na Katavi ni 5.9 kiwanga ambacho ni kikubwa kuliko wastani wa taifa wa asilimia 5.1.

Alitanabaisha kuwa katika maambukizi hayo, wanawake ndiyo walioathirika zaidi kwa kuwa na maambukizi ya wastani wa asilimia 9.2 na wanaume asilimika 6.5 kwa takwimu za utafiti wa mwaka 2011-2012.

‘’Wanawake wanaopata zaidi ugonjwa huo ni wale wenye umri wa miaka kati ya 20 mpaka 30 kwasababu hao ndiyo wanakuwa kwenye mahusiano, kuolewa na kujifungua’’ alisema Dr. Mlokozi.

Aliongeza kwa kusema kwamba, tayari kuna mikakati ya elimu kwa lika hiyo ili kuweza kupunguza ushamiri wa maambukizi hayo ya VVU kwa wanawake.

Kuhusu mkoa wa Mbeya, alisema mkoa huo umeendelea kuathirika zaidi  na ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa watu kimaendeleo ikiwemo suala zima la uchumi ambapo baadhi ya wafanyabiashara na madereva wanaotumia barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na kwenda Zimbabwe, Malawi, Zambia, Kongo na kwingineko kusini mwa Afrika, wanalala katika mkoa huo na kujiingiza katika mahusiano na baadhi hawatumii Kondomu.

‘’Nchi hizo zina maambukizi kuliko ya hapa nchini, hivyo pia ni moja ya sababu ya kuendelea kushamiri ugonjwa huo mkoani Mbeya na baadhi ya wanaume hawajafanyiwa tohara ambayo inasaidia kupunguza maambukizi kwa asilimia 60 na magonjwa ya zinaa’’ alisema Dr. Mlokozi.

VIFO VYA WAJAWAZITO TANZANIA, SAWA NA AJALI TANO ZA NDEGE ZA ABIRIA KILA SIKU

Mkurugenzi wa mradi wa Evidence for Action Craig Ferla akizungumza na waandishi wa habari Tanzania wanaobobea kuandika habari za afya ya uzazi2012.

NA, GORDON KALULUNGA.

INATIA moyo kusoma makala hii ambayo inatoa mchango wake katika kuhamasisha jamii ya watanzania kufahamu ukubwa wa changamoto zinazowakabili mama zetu na vichanga wakati wa ujauzito na kujifungua.

Katika tukio hilo adhimu la kuleta uhai duniani inasikitisha mno kwamba akina mama na watoto wachanga wengi hufariki hapa nchini.

Ni muhimu pia kutolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya taarifa zilizomo kwenye makala hii.

Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa wanawake 8,500 na watoto wachanga 50,000 hapa Tanzania hufariki kila mwaka katika kipindi cha ujauzito na kujifungua. Ni takwimu za kushtusha sana.

Ni muhimu kufafanua zaidi kuwa mtoto mchanga ni mwenye umri wa tangu siku 0 hadi 28, ikiwa ni pamoja na wanaozaliwa wameisha kufa.

Kuna idadi nyingine kubwa zaidi ya watoto walio chini ya miaka mitano ambao hufariki kila mwaka (kama ilivyojumuishwa kwa makosa kwenye makala hii, badala ya vichanga peke yake).

Ila izingatiwe kuwa vifo vya watoto katika siku 28 za kwanza za kuishi ni karibu theluthi moja ya vifo vyote vya watoto chini ya miaka mitano hapa Tanzania.

Ukichukua takwimu za wastani wa wanawake 8,500 na vichanga 50,000 wanaofariki wakati wa ujauzito na kujifungua kila mwaka nchini Tanzania, hii ni sawa na akina mama 23 na vichanga 137 wanaofariki kila siku.

Hili ni janga, hasa ukizingatia kuwa wengi wa akina mama na vichanga hawa wangeweza kuokolewa kama wangepata huduma bora.

Hata hivyo ni vigumu kuona na kuzingatia uhalisia wa kiwango na wingi wa vifo hivi katika maisha ya kila siku, hasa pale takwimu kubwa kama hizo zinapotumiwa.

Hivyo basi ndiyo sababu ukawekwa mfano huu kueleza ukubwa wa janga hili la kuwapoteza mama zetu na vichanga kila siku.


Ukisafiri ndani ya Tanzania kwa usafiri wa anga, kawaida ndege zinazotumika ni zile zenye kubeba abiria wapatao 30 hivi.

Na ndipo tulipoona muafaka kutumia mfano wa vifo vya akina mama 23 na vichanga 137 kila siku, kuwa ni kama ndege tano za abiria zingeanguka kila siku, ambapo kati ya hizo ndege tano, ndege moja ingebeba akinamama na nyingine nne zingebeba vitoto vichanga.

Kuielezea hali kwa namna hii ni kwa nia ya kufikisha ujumbe wa ukubwa wa janga hili linalozikumba familia na taifa kwa ujumla kila siku.

Hebu fikiria kama kungekuwepo kweli na ajali tano za ndege kila siku—kungekuwa na taharuki kubwa sana na wanajamii wa ngazi zote kulikemea jambo hili kudai likomeshwe mara moja, huku juhudi za kila aina zingefanywa lisitokee tena.

Ili kuboresha hali ya uzazi salama kwa kiwango kikubwa, ni muhimu sana wanawake wengi zaidi watafute nakupata huduma bora.

Iwapo kila mama atajifungulia kwenye kituo cha tiba ambacho kinatoa huduma bora, akina mama wengi na vichanga tunaowapoteza kwa sasa wataokolewa. Kwa sasa wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya bado ni wachache:

kwa mujibu wa utafiti wa Demografia na Afya Tanzania (TDHS) 2010 ni mwanamke mmoja tu katika kila wawili ndiye anayejifungulia katika kituo cha afya.

Yaani kigezo cha hatua hii muhimu ambayo ingeweza kuchukuliwa na kupunguza vifo vya mama na vichanga kwa kiasi kikubwa kimekuwa hivyo hivyo katika kipindi cha miaka 25 bila mabadiliko.

Hii ni tangu ulipofanyika utafiti wa TDHS wa kwanza 1990 ambapo ni nusu tu ya wanawake walikuwa wakijifungulia kwenye vituo vya afya.

Na japo kwa usahihi kabisa, makala hii imeeleza kuhusu ongezeko la idadi ya vizazi hai katika vituo vya afya, ieleweke kuwa pia ongezeko kubwa la idadi ya watu hapa Tanzania linamaanisha kuwa mfumo wa afya nao haujaweza kufanya mabadiliko ya kuendana na kiwango cha ongezeko la wanawake wanaojifungulia vituo vya afya kati ya mwaka 1986 na 2010.

Ujumbe mkuu hapa ni kuwa idadi kubwa ya akina mama na watoto wachanga wa Tanzania ambao maisha yao yanapotea wakati wa ujauzito na kujifungua kila mwaka yangeweza, na kwa hakika yanatakiwa kuokolewa.

Kila mtu, kwa nafasi yake katika jamii ni lazima atambue fursa zilizopo, zinazoweza kugeuza mwelekeo wa janga hili linalotokea kila siku.

Jitume, chukua hatua kuhakikisha mama zetu na vichanga wetu wanavuka salama kipindi hiki muhimu cha kuleta uhai.

USAFIRI HUU NI HATARISHI KWA WAJAWAZITO CHUNYA MBEYA


MIMBA ZA UTOTONI, KIKWAZO KWA WASICHANA MBEYA, PWANI NA MARA

WAKATI imebakia miaka miwili kuhakikisha malengo ya milenia yanatekelezwa, baadhi ya watoto wa kike nchini Tanzania, wamekuwa wakifukuzwa shule kutokana na ujauzito, huku wengine wakiacha wenyewe masomo pale tu wanapojigundua ni wajawazito.

Maeneo ambayo ymebainika kuwepo kwa hatari hiyo inayoendelea kwa watoto hao wa kike ni wilayani Ileje, Kyela mkoani Mbeya, Musoma mkoani Mara na Bagamoyo mkoani Pwani.

VIFAA TIBA, VYATOLEWA KWA MKOA WA MBEYA NA TANGA KWA AJILI YA MRADI WA AFYA YA MAMA NA MTOTO UNAOTEKELEZWA KWA USHIRIKIANO WA MFUKO WA TAIFA BIMA YA AFYA (NHIF) NA BENKI YA MAENDELEO YA WATU WA UJERUMANI-kfw


 
 VIFAA HIVYO NA MAJINA YAKE LA,A VINAVYOONEKANA. Vimekabidhiwa leo rasmi katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanywa na Waziri wa Afya, Dr. Seif Rashid, mkoani Mbeya.














 Kulia ni Mratibu wa afya ya mama na mtoto, Prisca Butuyuyu, akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa bima ya Taifa ya bima ya Afya Hamis Mdee(kushoto), katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya mradi wa KFW.

FAIDA ZA WAJAWAZITO KUJIFUNGULIA VITUO VYA AFYA HIZI HAPA

IKIWA mkoa wa Mbeya una asilimia 57 ya wajawazito wanaojifungulia hospitali na vituo vya afya, wito umetolewa kwao kujitokeza kwa wingi kuhudhuria Kliniki ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mhadhiri, kaimu mkuu wa taasisi ya tiba ya St. Aggrey Jijini Mbeya, Dr. Karim Segumba.
 
Dr. Karim alisema kuwa faida wanazozipata wajawazito wanapohudhuria Kliniki ni pamoja na mjamzito kuchunguzwa afya yake kwa undani, ikiwemo umri wa mimba, kimo cha mimba, historia ya uzazi wa awali, uwingi wa damu, mkojo kwa protini na kutoa wasiwasi wa kifafa cha mimba.

‘’Mwanamke anachunguzwa shinikizo la damu, mlalo wa mtoto, mapigo ya moyo ya mtoto, ikibidi ultrasound kuangalia kama mtoto yupo hai, au ni mlemavu, ukubwa wa mtoto, kondo la nyuma la mama, kukomaa kwa mtoto, nyonga za mama kama zinaruhusu kujifungua kwa njia ya kawaida au upasuaji na anaelezwa tarehe ya makisio ya kujifungua’’ alisema Dr. Karim.
Mbali na uchunguzi huo, alisema kuwa mjamzito anayehudhuria kliniki anapimwa pia VVU na anapoonekana kuwa ana maambukizi anapewa mbinu za kumkinga mtoto aliye tumboni.

Alipoulizwa madhara yanayoweza kuwapata wajawazito ambao hawaendi kliniki na hawajifungulii hospitali na vituo vya afya, alisema ni pamoja na mjamzito kutoelewa maendeleo ya mimba yake na hatari ambazo zingeweza kugundulika na kutatuliwa na wataalam ili kuzuia kifo chake na mtoto.

‘’Hivyo ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ni muhimu wajawazito wakahudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya tiba na kizuri zaidi huduma zote hizo kwa mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano hutolewa bure kote nchini’’ alisema mhadhili huyo.

Mratibu wa huduma ya mama na mtoto katika hospitali ya mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu, alisema kwa sasa mkoa wa Mbeya, wajawazito wengi wanahudhuria kliniki lakini wengi wao wanajifunguli nyumbani.

Aliitaja wilaya ya Ileje kuwa ndiyo wilaya inayoongoza kwa wajawazito kujifungulia nyumbani, ambapo Jiji la Mbeya linaongoza kwa wajawazito wengi kujifungulia katika vituo vya tiba.

‘’Zaidi ya asilimia 40 wajawazito wanajifungulia nyumbani lakini baadhi wanajifungulia kwa wakunga wa jadi na njiani ingawa hatuna takwimu sahihi zaidi’’ alisema Butuyuyu.

Alisema Jiji la Mbeya wajawazito wanajifungulia hospitali hasa hospitali ya wazazi Meta kwa asilimia 109, Kyela 67, Chunya 58, Rungwe 55, Mbozi 45, Mbeya Vijijini asilimia 38 na wilaya ya Ileje asilimia 33.

WAJAWAZITO TANZANIA WAJIFUNGULIA MALAWI

TUJIKUMBUSHE MAKALA HII NA KUTAFAKARI

*Unafuu na kutotozwa fedha wala vifaa, kivutio tosha.
Na Gordon Kalulunga.
SERA ya Afya ya mwaka 2007 haifahamiki wilayani Ileje katika mkoa wa Mbeya. Ni katika sera hii ambamo inatamkwa kwamba wajawazito nchini watapewa huduma za afya bure.


Kama sera inafahamika, basi haitekelezwi. Baadhi ya wajawazito katika wilaya ya Ileje wanaacha zahanati, vituo vya afya na hospitali wilayani mwao na kuvuka mpaka hadi nchini Malawi kufuata kinachoitwa “huduma bora.”


Kwa mfano, wajawazito kutoka kata za Bupigu, Itumba na Isongole wanafahamika kwa kwenda nchini Malawi kwa wingi ili waweze kujifungulia huko na kupata huduma nyingine za afya.


Lakini kutoka Isongole hadi hospitali maarufu ya Chitipa nchini Malawi ni umbali wa kilometa 45; wakati umbali wa kwenda hospitali ya serikali ya Ileje ni kilomita tatu tu.


Mwanamke mkazi wa kijiji cha Ikumbilo, kata ya Chitete wilayani Ileje, aliyejitambulisha kuwa anaishi na virusi vya ukimwi (VVU) anasema aliwahi kujifungulia hospitali ya Chitipa na mpaka sasa anapata matibabu yake huko.


Kuna nini katika hospitali ya Chitipa nchini Malawi hadi wajawazito wakimbilie huko? Jibu analo Neema Mbughi mkazi wa kijiji na kata ya Bupigu.


“Pale hospitali ya Chitipa hubebi chochote wakati unakwenda kujifungua. Hatuendi na madishi, karatasi za nailoni (ambako mjamzito huhala wakati wa kujifungua) wala glovu. Kila kitu ni bure, hata chakula ambacho kimepikwa kama kimetoka nyumbani,” anaeleza Neema.

Friday 30 May 2014

DALILI 13 ZA MWANAMKE MJAMZITO


by Gordon Kalulunga

 
TANGU niwe mmoja wa waandishi wa habari 5 waliobahatika kufauru usaili kati ya waandishi 72 Tanzania na kujifunza na kubobea kuandika habari za afya ya uzazi nchini Tanzania tangu mwaka 2012 nimejionea, nimesikia, nimegusa, nimenusa wakati mwingine kuyaishi maisha na wanawake wajawazito na hata ambao bado hawajawa wajawazito.


Nieleze wazi kuwa mafunzo hayo niliyapata kupitia program ya Fellowship inayoratibiwa na mfuko wa vyombo vya habari Tanzania maarufu kama Tanzania Media Fund (TMF) na kufundishwa na madaktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi.



Moja ya mambo ambayo nilijifunza kutoka kwa wataalamu hasa madaktari nikiwa field, kusoma mitandao na baadhi ya wanawake waliosema wazi wazi kuhusu dalili za ujauzito na kati ya nyingi nilizoelezwa kati yake 13 nimeona nikushirikishe katika makala hii ya uchambuzi.


Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

 Inaonesha kuwa homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa katika mwili wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi wa kujua kama mjauzito au la.


 1. Maumivu kwenye matiti.
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

2. Maumivu mwilini
Baadhi ya wznawake wanajisikia maumivu kama vile wanataka kuingia katika siku zao. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.


3. Kutokwa damu bila kutegemea
Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai na iwapo utaona hedhi inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, mwanamke anashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito au kujipima mwenyewe na kifaa cha kupimia ujauzito..


4. Kuchoka
Mwanamke anapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati akiwa kazini, wakati huo mwili wake unakuwa unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

 Inaelezwa kuwa katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu za mwanamke na hivyo kumletea uchovu na usingizi.


5. Chuchu kuwa nyeusi
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi hata hivyo wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.


6. Kichefuchefu
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

7. Mwili kuvimba


Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kumsababishia mwanamke kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinambana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.


8. Kwenda haja ndogo mara kwa mara
Mwanamke kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito.


Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

 9. Tamaa ya vitu mbalimbali.
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.


 10. Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.



11. Kufunga choo.
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
  

12. Kuwa na hasira
‘’Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.


13. Kuongezeka kwa joto mwilini.
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.

0754 440749

MAMBO MUHIMU AMBAYO UNATAKIWA UYAFANYE KABLA YA KUOA AU KUOLEWA



Dr, Pastor, Gordon Kalulunga.

MOJA ya mambo ambayo yanakosekana katika nyumba za ibada ni mafundisho ya mahusiano.

Watu wengi hawajui kuwa mtu aliyeolewa na hajaolewa au kuoa, ana haki ya kupata elimu ya ndoa.

Unaweza kujiuliza kuwa kwanini ndoa nyingi zina shida? Jawabu ni kwamba wengi wanajua ndoa baada ya kuingia kwenye ndoa, hawajawahi kupata elimu ya mahusiano.

Ni sawa na kumfundisha dereva kuendesha gari.

Wengi wamekosa elimu ya mahusiano au kuoa au kuolewa, vijana na mahusiano, bali wengi wana elimu za upako wa mafanikio na toa ndugu toa ndugu ndiyo masomo tuliyoyazoea.

Mfumo wa elimu tuliyonayo nao ni tatizo. Kwa mfano kwenye Biblia hakuna neno linalosema rafiki au mchumba.

Huwezi kukuta kitu kinachoitwa, urafiki, uchumba baadaye ndoa.
Ngoja nikuambie, Mathayo Mtakatifu sura ya 1;1-23. Mariamu alipoposwa….. haisemi alichumbiwa! Lakini katika utamaduni wa kimagharibi leo hii watu wanasema kuwa mchumba wa Yusufu.

Mchumba huwa anapimwa, ndiyo maana watu wanakuwa na wachumba wengi kweli na hatimaye uchumba unavunjika kwasababu hakuna mtu anayeenea kwenye utimilifu.

Kuna fix za kifikra ambazo zina ugonjwa wa kufisha, kesho unaweza kulia ukiendekeza kumtafuta mchumba badala ya kumtafuta mume au mke.

Akina dada wengi wanaomba na kusugua magoti wakiomba wapate wachumba.

Maandiko yanasema kuwa, ‘’Mjibu mpumbavu kutokana na upumbavu wake’’
Mtu ana wachumba kadhaa, kisha anaanza kumuomba Mungu ampe mume au mke huku akiwa na vinyago vyake. Majibu yatakuja kama anavyowaza. 

Yaani tayari wana fikra, vinyago na maamuzi yao kati ya wale wachumba waliopo moyoni na kichwani.

Mungu atamjibu mtu kutokana na elimu aliyonayo ya urafiki, uchumba kisha ndoa.

 Walio kwenye ndoa wengi wanajuta kwasababu wameoa au kuolewa na rafiki….

Ukikaa na mtu utasikia anakuambia, mtumishi nimeumia, tunakuabudu Bwana, utafikiri upako umetembea, kumbe watu wana kesi zao na nafsi zao zimepigwa.

Mimi kama mwalimu ambaye sawa na Daktari, nikianza kufuatilia ninajua.
Ukimuuliza vipi ina maana una chimichimi ya roho mtakatifu ndiyo maana kila tunapoanza kuabudu analia?

Ukidadisi mtu anakumbia kuwa, nilikuwa na mchumba akaniambia utanioa, akamwambia na rafiki yangu na mwingine…..

Nafsi za watu wa Mungu nyingi zimeumizwa na kuna kesi nyingi za kuachwa kuliko kesi za uhalifu mwingine.

Ukiomba mchumba, wanaweza kuja wengi kisha unapoanza kuburuzana nao unachoka kisha unatumbukia popote…..

Jambo hili la ndoa na uchumba ni gumu kwasababu vijana wengi ni wavivu kujifunza maandiko ya Mungu bali wanataka watafuniwe kila kitu na kulishwa.

Mungu ni roho, alimuumba mtu kwa mfano wake, akasema nendeni duniani mkazae na kuongezeka. Maandiko yanaposema Mtu, ina maanisha mfano wa roho.

Kwenye ulimwengu wa roho, Mungu aliumba mtu mke na mtu mume na ndiyo maana amekataza kuzini.

Maana yake ni kwamba kila mmoja ana mke wake na ana mume wake kwasababu kila mmoja aliumbwa na wake.

Ukiishika elimu hiyo, hautalia kwasababu eti hujapata mume au mke. Mbinguni kuna roho nyingi zinazataka kuja duniani, hivyo tuliopo tumepata neema ya kutangulia kuzaliwa.

Unapomuona mwanaume anapita, ujue kuwa huyo ni mume wa mtu na mwanake anayepita ni mke wa mtu.

Tatizo watu wanaomba kwa Mungu wapate mke au mume huku wakilia! 

Inashangaza mtu unaenda kudai deni lako huku akilia. Maana yake hajui haki yake, yaani imani zetu hazijawa sawa.

Kama ndani yako una usongo wa kuoa au kuolewa, fanya hivi. Kwa imani nenda kamnunulie na suti iweke ndani maana kwa imani yupo. 

Acha kushika yeyote mwisho utashika hata majoka.
Mungu hupendezwa na mtu mwenye imani na anamletea. Acha kulia.

Wanaume ngoja niwaambie. Mungu alipokuwa akiumba, alimtanguliza Brother men, kisha akamlaza usingizi na kuchomoa ubavu akamtengeneza mwanamke. Maana yake ni kwamba mwanamke wa kwako yupo, labda uwe towashi.

Wanawake hampaswi kufifia ngozi kwamba hamtaolewa, maana usigeweza kuumbwa bila wa kwako kuwepo na wala hajafa bali yupo, cha kufanya amini. Kanunue na suti kaweke ndani, anza kufanya maandalizi…

Kuweni na imani inayowekwa kwenye matendo, msiamni kuwa mtakosea.
 
Sehemu nyingine huwa nawafundisha kuwa, ukishatambua kuwa wa kwako yupo, tulia au subiri.

Kwa kuwa hatuamini kuwa wa kwako yupo, hatutulii, na kwa kuwa tunaanza kaba ya majira na wakati ndipo tunapoeekea kwenye kuumia na majuto ya uchumba na ndoa.

Wimbo uiobora 3;5 ….msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha……Mungu anasema hayo kwasababu kabla ya Mungu kuyaamsha, wewe unawahi.

Mfano; Sekondari mtu hasa wanawake, anapokuwa kidato cha pili tu au kabla ya hapo, anaanza kuomba, Mungu nipe Mume….. hebu jiulize wewe ulianza lini kuzitikisa mbingu za mapenzi…… jibu unalo.

Wanyakyusa wanao usemi kwa mtu mzima anayefanya mambo ya hovyo, unasema…..amakambo, akwesile ndili… yaani mtu huyo anasumbuliwa na bangi….alivuta lini?

Hapa namaanisha kuwa unaweza kukimbilia na ukapata mume maana hakuna mtu anayekuwa anazijua tabia za wenzake, kisha utaanza kusema kuwa aaaaa…kumbe hakuwa mwenyewe..

Ibrahimu haraka zake zinasumbua kule Israel mpaka leo.
 
Niwaambie ukweli kuwa haraka zina hasara zake sawa na utunzaji wa mtoto njiti ni kazi kubwa. 

Hivyo ukiharakisha unaweza kupata mume au mke njiti…

Sijui kama ninaeleweka katika somo hili. Haraka zinaendana na akina dada kuongea harakaharaka, wanaume wengi hawapendi mwanamke wa namna hiyo.

Yesu aliwahi kujaribiwa na kahaba, mafarisayo miili yao ikawa nyang’anyang’a huku yule kahaba akitoa machozi na kufuta miguu ya Yesu kwa nywele zake, hivi ungekuwa wewe Brother men ungefanyaje hapo?

Usiwe na haraka. Watoto wa kike ndo wana speed kuliko hata dunia inavyozunguka jua.

Hamnoni alimpenda Tamali mpaka akaumwa…. Lakini baada ya kulala naye akamchukia na kumwambia Tamali aondoke na akamchukia kwelikweli…..tafakari.

Hapa kinachotendeka katika ulimwengu wa roho ni kependa umbo lakini my akionja hakuti kile ambacho alikuwa anakifikiri.

Mfano mzuri ni kwamba wanaume na wanawake wengi ambao wamedumu katika mapenzi hawaoani.

Mwanaume akitembea na mwanamke na kutokukuta alichokitarajia, anasema hata kwa wenzake kuwa ‘’demu mwenyewe mshamba na hana lolote’’ yote hiyo ni kuyachochea mapema na kuvua.
 
Nitajuaje kama ndiye?

Kimaandiko unapomuomba Mungu, utawekewa rohoni kitu kinachoitwa mwongozo.

Utaona unasukumwa na jambo la kuolewa kama kuku navyosumbuka kutafuta eneo la kutagia, sawa na mtumishi wa Mungu anapotaka kufanya jambo la kiroho.

Jifunze kumsikiliza Mungu, ondoa moyoni kufikiri kuwa huyo unayefikiri na kumweka moyoni kama ni mwenyewe, huyo siyo. 

Achana naye maana roho ya mauti ipo juu yako. Tubu.  

MSIKILIZE MUNGU ILI ASIKUJIBU SAWA SAWA NA VINYAGO ULIVYOWEKA MOYONI MWAKO NA KUJIINGIZA POPOTE. 

HEBU JIULIZE, MPAKA SASA UNA VINYAGO VINGAPI?
Hili ni somo la sikio halisi, siku nyingine nitatoa mifano yangu halisi…..
 
Mungu awabariki na awasamehe wote wenye toba.


Gordon Kalulunga
Information and Media Consultant
P.O. Box 705, Mbeya-Tanzania
Tel: 255 (0)754 440749
WEB; www.kalulunga.blogspot.com