Sunday, 21 December 2014
Saturday, 20 December 2014
SIRI YA HERUFI YA MWANZO YA JINA LAKO
HERUFI A
HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.
HERUFI G
Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni
mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha
kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia
kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.
HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.
HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.
HERUFI Y (YASINTA)
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha.
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.
KUELEKEA CHRISTMASS, UNGEJUA MUMEO/MKEO/MPENZI WAKO ATAKUWA NA TABIA ALIZONAZO JE UNGEMKUBALI?
1. Kama ungejua mumeo au mkeo atakuwa na tabia aliyonayo sasa ugekubali kuoana naye?
2. Je umeoa/kuolewa na mtu uliyemtaka; ni chaguo lako halisi?
3. Sababu gani zinakufanya uendelee kuishi na mkeo/mumeo hadi sasa Je (watoto, sababu ndoa ya kikristo haina talaka/wazazi watakulaani ukitengana nae/navumilia/bado nampenda/ tunaishi kwa mazoea?)
4. Sababu gani iliyokufanya uwe na uhusiano wa kingono nje ya ndoa?(kuchuja kwa mwenzako, tamaa ya mwili, marafiki wabaya, kasoro ya kimaumbile ya mwenzangu, tamaa ya mali/ kukosekana kwa maelewano ndani ya nyumba).
Majibu bila shaka unayo lakini tunaweza kukusaidia zaidi....
Teta nami
Brother Kalu
0655 440749
kalulunga2006@gmail.com
2. Je umeoa/kuolewa na mtu uliyemtaka; ni chaguo lako halisi?
3. Sababu gani zinakufanya uendelee kuishi na mkeo/mumeo hadi sasa Je (watoto, sababu ndoa ya kikristo haina talaka/wazazi watakulaani ukitengana nae/navumilia/bado nampenda/ tunaishi kwa mazoea?)
4. Sababu gani iliyokufanya uwe na uhusiano wa kingono nje ya ndoa?(kuchuja kwa mwenzako, tamaa ya mwili, marafiki wabaya, kasoro ya kimaumbile ya mwenzangu, tamaa ya mali/ kukosekana kwa maelewano ndani ya nyumba).
Majibu bila shaka unayo lakini tunaweza kukusaidia zaidi....
Teta nami
Brother Kalu
0655 440749
kalulunga2006@gmail.com
Dalili 13 za mwanamke mjamzito
by Gordon Kalulunga
TANGU niwe mmoja wa waandishi wa habari 5 waliobahatika kufauru usaili kati ya waandishi 72 Tanzania na kujifunza na
kubobea kuandika habari za afya ya uzazi nchini Tanzania tangu mwaka
2012 nimejionea, nimesikia, nimegusa, nimenusa wakati mwingine kuyaishi
maisha na wanawake wajawazito na hata ambao bado hawajawa wajawazito…
Nieleze wazi kuwa mafunzo hayo niliyapata kupitia program ya Fellowship
inayoratibiwa na mfuko wa vyombo vya habari Tanzania maarufu kama
Tanzania Media Fund (TMF) na kufundishwa na madaktari bingwa wa masuala
ya afya ya uzazi.
Moja ya mambo ambayo nilijifunza kutoka kwa wataalamu hasa madaktari
nikiwa field, kusoma mitandao na baadhi ya wanawake waliosema wazi wazi
kuhusu dalili za ujauzito na kati ya nyingi nilizoelezwa kati yake 13
nimeona nikushirikishe katika makala hii ya uchambuzi.
Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili
ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza
kuuchunguza mwili wake.
Inaonesha kuwa homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito
husababisha mabadiliko kadhaa katika mwili wake ambayo yanaweza
kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi wa kujua kama mjauzito au la.
1. Maumivu kwenye matiti.
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.
2. Maumivu mwilini
Baadhi ya wznawake wanajisikia maumivu kama vile wanataka kuingia katika siku zao. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.
Baadhi ya wznawake wanajisikia maumivu kama vile wanataka kuingia katika siku zao. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.
3. Kutokwa damu bila kutegemea
Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai na iwapo utaona hedhi inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, mwanamke anashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito au kujipima mwenyewe na kifaa cha kupimia ujauzito..
Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai na iwapo utaona hedhi inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, mwanamke anashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito au kujipima mwenyewe na kifaa cha kupimia ujauzito..
4. Kuchoka
Mwanamke anapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati akiwa kazini, wakati huo mwili wake unakuwa unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
Mwanamke anapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati akiwa kazini, wakati huo mwili wake unakuwa unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
Inaelezwa kuwa katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao
mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu za mwanamke na hivyo
kumletea uchovu na usingizi.
5. Chuchu kuwa nyeusi
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi hata hivyo wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi hata hivyo wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.
6. Kichefuchefu
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
7. Mwili kuvimba
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza
kumsababishia mwanamke kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinambana
kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na
ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una
ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
8. Kwenda haja ndogo mara kwa mara
Mwanamke kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito.
Mwanamke kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito.
Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu
kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa
muda mrefu.
9. Tamaa ya vitu mbalimbali
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.
10. Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.
11. Kufunga choo.
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
12. Kuwa na hasira
‘’Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.
‘’Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.
13. Kuongezeka kwa joto mwilini
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito.
Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa
linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa
inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.
0754 440749
JE UNA UFAHAMU MZURI KUHUSU KONDOMU NA UKIMWI? SOMA HAPA

Kondomu hizi
zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa, nazo ni kama
ifuatavyo:-
Awamu ya I –
zilizotengenezwa kwa mimea.
Hizi
zilitengenezwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa
wa kaswende [ugonjwa wa kifaransa]
Awamu ya II
– kutokana na utumbo wa kondoo.
Dr. Condom
alifahamika kama mgunduzi wa kondomu hizi, naye alikuwa ni dakatari wa Mfalme
Charles II.
Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.
Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.
Awamu ya III
– kutokana na mpira
Hizi
zilitengenezwa kwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa
kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira.
JE KONDOMU
NI SALAMA?
Tunaelezwa
kuwa kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba haziwezi kuruhusu kitu
chochote kupita.
Lakini
tafiti mbalimbali zilizofanyika zinaonyesha kuwa kondomu zaweza kuvuja kutokana
na mazingira halisi ya utengenezaji wa latex.
Wengine
wanadai kuwa ili kuzifanya imara, kondomu zimetengenezwa kwa kupishanisha pande
mbili ili kuziba udhaifu wa kila upande.
Hata hivyo
watengenezaji wanasahau kuwa mazingira ya matumizi ya kondomu katika ngono
hayalingani na majaribio waliyofanya ya kujaza maji au hewa ili kupima kama
maji na hewa vinapita.
Katika tendo
la ngono ipo misuguano ya namna mbalimbali inayosababisha kubadilisha mazingira
ya kondomu na kuidhoofisha.
Kutokana na
tafiti hizo imefahamika kuwa kondomu hazina uwezo wa kuzuia mbegu za kiume
kupenya wakati wote.
Upana wa
kipenyo cha mbegu ni makroni 5 wakati upana wa kipenyo cha kirusi cha ukimwi ni
makroni 0.1
Kwa maneno
mengine mbegu ya kiume ni kubwa mara 50 ya kirusi cha ukimwi.
Vile vile
tafiti zimeonyesha kuwa kondomu haina uwezo wa kuzuia maambukizo ya magonjwa ya
zinaa vikiwemo virusi vya ukimwi kwa kiwango cha asilimia mia moja.
Hivyo tunaweza kusema kuwa, kondomu si salama
kwa asilimia mia moja.
Kondomu zina
kiwango cha kushindwa cha kati ya asilimia 10 na 15 na wengine wanasema hata
asilimia 20.
Wasambazaji
na wahamasishaji wa matumizi ya kondomu hawapendi kusikia ukweli huo na
wanafanya jitihada kubwa ya kuficha ukweli huo.
Matangazo
yatolewayo kupitia mabango ya barabarani, katika televisheni, radio na hata
magazeti yanawarubuni watu yakiwaaminisha kuwa kondomu humkinga mtumiaji kwa
kiwango cha asilimia 100%
Huko ni
kukengeusha ukweli na kukiuka maadili ya kitaaluma.
Wengi kama
sio wote wateteao matumizi ya kondomu hufanya hivyo kwa sababu ya maslahi ya
kifedha na kibiashara.
Tukiongozwa
na dhamiri safi, lazima tukiri ukweli uliopo na tuwaeleze watumiaji, ili
tusijekuwa sababu ya kifo chao.
Kila kondomu
inaposhindwa [itumikapo] kama kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya ukimwi ]
humaanisha kifo.
Udhaifu wa kondomu Kiufundi,Matumizi, Kimazingira
Udhaifu wa kiufundi
Wasambazaji
wanatueleza kuwa kondomu zilizotoka kiwandani zikiwa na ubora unaotakiwa
zikitumika wakati wote na kwa usahihi zina uwezo wa kukinga kwa kiwango hadi
cha asilimia 97.
Zisipotumika
vizuri zina kiwango cha kushindwa cha asilimia 14.
Kiwango cha
kushindwa kwa kondomu kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa hutofautiana
kutokana na aina ya magonjwa ya zinaa.
Kondomu
zaweza kuzuia kwa kiwango fulani maambukizo ya magonjwa ya zinaa yanayosafiri
kwa njia ya ute, lakini haziwezi kuzuia magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa
mgusano wa mwili kama vile "herpes" na "human
papillomavirus"; au magonjwa yanayoambukizwa kutokana na vidonda au
malengelenge yaliyoko kwenye via vya uzazi kama vile kaswende.
Hali hiyo
inatokana na:
Watengenezaji
wameruhusu udhaifu wa kiufundi kama zao la kiwandani lililotengenezwa na kazi
ya mikono ya binadamu [acceptable quality limit] kwa kiwango Fulani kwa nchi
mbalimbali.
Mfano,
Marekani kiwango kilichokubaliwa ni asilimia 99.6 kwa kutoruhusu kondomu
kuvuja.
Uingereza asilimia 97, Uholanzi asilimia 96. 5. Hivyo katika kila idadi ya kondomu itumikayo kwa wakati mmoja kuna kiwango cha kuvuja kati ya asilimia 0.4 (USA); 3% (Britania); 3.5% (Holland).
Uingereza asilimia 97, Uholanzi asilimia 96. 5. Hivyo katika kila idadi ya kondomu itumikayo kwa wakati mmoja kuna kiwango cha kuvuja kati ya asilimia 0.4 (USA); 3% (Britania); 3.5% (Holland).
Kondomu huzeeka
Kwa kadiri
zisivyotumika kwa muda mrefu ndivyo hivyo zinaaendelea kuzeeka.
Kwa hiyo
mtumiaji kondomu wa miaka 3 au 4 baada ya kondomu hiyo kutengenezwa yumo katika
hatari zaidi kuliko anayetumia kondomu mara tu baada ya kutoka kiwandani.
Utafiti
mmoja umeonyesha kuwa kiwango cha kupasuka kwa kondomu kiliongezeka kutoka 3.6%
kwa kondomu mpya hadi 18.6% kwa kondomu zilizotumika miaka kadhaa baadaye.
Kondomu hupasuka.
Kiwango cha
kupasuka hutegemea aina ya kilainisho kilichotumika na aina ya kondomu. Kwa
mujibu wa tafiti 15 zilizofanywa na "Contraceptive Technology"
yalionyesha kuwa katika kondomu 25,184 zilizotumika 4.64% zilipasuka.
Ingawaje
kondomu za latex zinaonekana kuwa na kiwango kidogo sana cha kupitisha virusi vya
ukimwi, hatari kubwa ya matumizi yake imo katika uwezekano wa kondomu kupasuka,
kuteleza na kuteleza.
Kwa hiyo
hata kama ni virusi vichache tu vinaweza kupenya, kiwango cha maambukizo
kitakuwa kikubwa kadiri kondomu zinavyosambazwa kwa wingi na kadiri watu
wanavyojihusisha na vitendo vya ngono wakiamini katika matumizi ya kondomu.
Udhaifu
katika matumizi
Matumizi mabaya: yaani kutovaa vizuri,
kuvaa nje ndani, aina ya ngono, urefu wa muda wa ngono, pia kutokana na uelewa
mdogo hasa kwa wasojua kusoma na kuandika na wale wakaao mbali na mijini.
Kuteleza na kuvulika kutokana na hali ya
uume kuwa mdindifu au la; upana au wembamba; mrefu au mfupi.
Pia kutokana
na tendo la ngono na hali ya mtumiaji na mazingira ya matumizi.
Kutokana na umri wa mtumiaji, kama ni mtoto, kijana, mtu mzima au mzee.
Kutokana na umri wa mtumiaji, kama ni mtoto, kijana, mtu mzima au mzee.
Kutumia
kondomu ambazo muda wake umepita. Mfano wanaotumia gizani , katika hali ya
ulevi, kutokujua kusoma, kuchunguza na kugundua kama muda wake umepita.
Mazingira ya
kingono yakishawekwa, watu wanatawaliwa na mihemuko ya juu ya ngono kiasi
kwamba hawawezi kuchunguza tarehe ya ukomo wa matumizi ya kondomu.
Ingawa
watengenezaji wanashauri kutotumia kondomu iliyobadilika rangi au iliyokauka,
tabia za watumiaji hazina nafasi ya kuzingatia ushauri huo.
Lengo la
mtumiaji laweza kusababisha matumizi kuwa mabaya. Mtu mwenye virusi vya ukimwi,
anajiwekea lengo kwamba hataki kufa peke yake, atafanya jitihada za kutokutumia
vizuri ili mwenzake [ambaye anaamini hajaambukizwa] aweze kuambukizwa ili,
"nisife peke yangu".
Vilevile
katika siku hizi za dawa za kupunguza makali ya kuzaliana virusi vya ukimwi,
mtu anaweza kuonekana mwenye afya nzuri kabisa, na anaweza kumshawishi mwenzake
kuachana na kondomu kwa vile "wanaaminiana".
Kwa hiyo
mambukizi yanaweza kuwa makubwa kutokana na kutowadhibiti wale waliokwisha
ambukizwa.
udhaifu wa kimazingira
Huu
unatokana na hali zifuatazo:- kibinadamu,
kimaumbile na Kibinadamu.
Udhaifu wa
kondomu waweza kusababishwa na usafirishwaji, yaani muda unaotumika kusafiri
kutoka sehemu zinapotengenezwa hadi mahali zinapotumika;
ii.
Kimaumbile
Vyombo vya
usafirishaji na usalama wa vyombo hivyo;
Kondomu
zinazosafirishwa katika meli, zikiwa baharini kwa miezi kadhaa kabla hazijafika
katika nchi lengwa na katika hali ya joto ndani ya makontena zinakuwa na
kiwango hafifu katika ubora wake.
Udhaifu wa
sehemu ya kuhifadhi kondomu pamoja na vyombo vya kuhifadhia.
source.
Human Life International.
Gordon
Kalulunga,
Information
and Media Consultant
P.O. Box
705, Mbeya-Tanzania
Tel: 255
(0)754 440749
e-mail: uhaiwamama@gmail.com
www.udakumsumari.blogspot.com
Friday, 19 December 2014
MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE KABLA YA KUOA AU KUOLEWA
MOJA ya
mambo ambayo yanakosekana katika nyumba za ibada ni mafundisho ya mahusiano.
Watu wengi
hawajui kuwa mtu aliyeolewa na hajaolewa au kuoa, ana haki ya kupata elimu ya
ndoa.
Unaweza
kujiuliza kuwa kwanini ndoa nyingi zina shida? Jawabu ni kwamba wengi wanajua
ndoa baada ya kuingia kwenye ndoa, hawajawahi kupata elimu ya mahusiano.
Ni sawa na
kumfundisha dereva kuendesha gari.
Wengi wamekosa
elimu ya mahusiano au kuoa au kuolewa, vijana na mahusiano, bali wengi wana
elimu za upako wa mafanikio na toa ndugu toa ndugu ndiyo masomo tuliyoyazoea.
Mfumo wa
elimu tuliyonayo nao ni tatizo. Kwa mfano kwenye Biblia hakuna neno linalosema
rafiki au mchumba.
Huwezi
kukuta kitu kinachoitwa, urafiki, uchumba baadaye ndoa.
Ngoja
nikuambie, Mathayo Mtakatifu sura ya 1;1-23. Mariamu alipoposwa….. haisemi
alichumbiwa! Lakini katika utamaduni wa kimagharibi leo hii watu wanasema kuwa
mchumba wa Yusufu.
Mchumba huwa
anapimwa, ndiyo maana watu wanakuwa na wachumba wengi kweli na hatimaye uchumba
unavunjika kwasababu hakuna mtu anayeenea kwenye utimilifu.
Kuna fix za
kifikra ambazo zina ugonjwa wa kufisha, kesho unaweza kulia ukiendekeza
kumtafuta mchumba badala ya kumtafuta mume au mke.
Akina dada
wengi wanaomba na kusugua magoti wakiomba wapate wachumba.
Maandiko
yanasema kuwa, ‘’Mjibu mpumbavu kutokana na upumbavu wake’’
Mtu ana
wachumba kadhaa, kisha anaanza kumuomba Mungu ampe mume au mke huku akiwa na vinyago
vyake. Majibu yatakuja kama anavyowaza.
Yaani tayari wana fikra, vinyago na maamuzi yao kati ya wale wachumba waliopo moyoni na kichwani.
Yaani tayari wana fikra, vinyago na maamuzi yao kati ya wale wachumba waliopo moyoni na kichwani.
Mungu
atamjibu mtu kutokana na elimu aliyonayo ya urafiki, uchumba kisha ndoa.
Walio kwenye ndoa wengi wanajuta kwasababu
wameoa au kuolewa na rafiki….
Ukikaa na
mtu utasikia anakuambia, mtumishi nimeumia, tunakuabudu Bwana, utafikiri upako
umetembea, kumbe watu wana kesi zao na nafsi zao zimepigwa.
Mimi kama
mwalimu ambaye sawa na Daktari, nikianza kufuatilia ninajua.
Ukimuuliza
vipi ina maana una chimichimi ya roho mtakatifu ndiyo maana kila tunapoanza
kuabudu analia?
Ukidadisi
mtu anakumbia kuwa, nilikuwa na mchumba akaniambia utanioa, akamwambia na
rafiki yangu na mwingine…..
Nafsi za
watu wa Mungu nyingi zimeumizwa na kuna kesi nyingi za kuachwa kuliko kesi za
uhalifu mwingine.
Ukiomba
mchumba, wanaweza kuja wengi kisha unapoanza kuburuzana nao unachoka kisha
unatumbukia popote…..
Jambo hili
la ndoa na uchumba ni gumu kwasababu vijana wengi ni wavivu kujifunza maandiko
ya Mungu bali wanataka watafuniwe kila kitu na kulishwa.
Mungu ni
roho, alimuumba mtu kwa mfano wake, akasema nendeni duniani mkazae na
kuongezeka. Maandiko yanaposema Mtu, ina maanisha mfano wa roho.
Kwenye
ulimwengu wa roho, Mungu aliumba mtu mke na mtu mume na ndiyo maana amekataza
kuzini.
Maana yake
ni kwamba kila mmoja ana mke wake na ana mume wake kwasababu kila mmoja
aliumbwa na wake.
Ukiishika
elimu hiyo, hautalia kwasababu eti hujapata mume au mke. Mbinguni kuna roho
nyingi zinazataka kuja duniani, hivyo tuliopo tumepata neema ya kutangulia
kuzaliwa.
Unapomuona
mwanaume anapita, ujue kuwa huyo ni mume wa mtu na mwanake anayepita ni mke wa
mtu.
Tatizo watu
wanaomba kwa Mungu wapate mke au mume huku wakilia! Inashangaza mtu unaenda
kudai deni lako huku akilia. Maana yake hajui haki yake, yaani imani zetu
hazijawa sawa.
Kama ndani
yako una usongo wa kuoa au kuolewa, fanya hivi. Kwa imani nenda kamnunulie na
suti iweke ndani maana kwa imani yupo. Acha kushika yeyote mwisho utashika hata
majoka.
Mungu
hupendezwa na mtu mwenye imani na anamletea. Acha kulia.
Wanaume
ngoja niwaambie. Mungu alipokuwa akiumba, alimtanguliza Brother men, kisha
akamlaza usingizi na kuchomoa ubavu akamtengeneza mwanamke. Maana yake ni
kwamba mwanamke wa kwako yupo, labda uwe towashi.
Wanawake
hampaswi kufifia ngozi kwamba hamtaolewa, maana usigeweza kuumbwa bila wa kwako
kuwepo na wala hajafa bali yupo, cha kufanya amini. Kanunue na suti kaweke
ndani, anza kufanya maandalizi…
Kuweni na imani
inayowekwa kwenye matendo, msiamni kuwa mtakosea.
Sehemu
nyingine huwa nawafundisha kuwa, ukishatambua kuwa wa kwako yupo, tulia au
subiri.
Kwa kuwa
hatuamini kuwa wa kwako yupo, hatutulii, na kwa kuwa tunaanza kaba ya majira na
wakati ndipo tunapoeekea kwenye kuumia na majuto ya uchumba na ndoa.
Wimbo
uiobora 3;5 ….msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha……Mungu anasema hayo kwasababu
kabla ya Mungu kuyaamsha, wewe unawahi.
Mfano;
Sekondari mtu hasa wanawake, anapokuwa kidato cha pili tu au kabla ya hapo,
anaanza kuomba, Mungu nipe Mume….. hebu jiulize wewe ulianza lini kuzitikisa
mbingu za mapenzi…… jibu unalo.
Wanyakyusa
wanao usemi kwa mtu mzima anayefanya mambo ya hovyo, unasema…..amakambo,
akwesile ndili… yaani mtu huyo anasumbuliwa na bangi….alivuta lini?
Hapa
namaanisha kuwa unaweza kukimbilia na ukapata mume maana hakuna mtu anayekuwa
anazijua tabia za wenzake, kisha utaanza kusema kuwa aaaaa…kumbe hakuwa
mwenyewe..
Ibrahimu
haraka zake zinasumbua kule Israel mpaka leo.
Niwaambie ukweli kuwa haraka zina hasara zake sawa na utunzaji wa mtoto njiti ni kazi kubwa. Hivyo ukiharakisha unaweza kupata mume au mke njiti…
Niwaambie ukweli kuwa haraka zina hasara zake sawa na utunzaji wa mtoto njiti ni kazi kubwa. Hivyo ukiharakisha unaweza kupata mume au mke njiti…
Sijui kama
ninaeleweka katika somo hili. Haraka zinaendana na akina dada kuongea
harakaharaka, wanaume wengi hawapendi mwanamke wa namna hiyo.
Yesu aliwahi
kujaribiwa na kahaba, mafarisayo miili yao ikawa nyang’anyang’a huku yule
kahaba akitoa machozi na kufuta miguu ya Yesu kwa nywele zake, hivi ungekuwa
wewe Brother men ungefanyaje hapo?
Usiwe na
haraka. Watoto wa kike ndo wana speed kuliko hata dunia inavyozunguka jua.
Hamnoni
alimpenda Tamali mpaka akaumwa…. Lakini baada ya kulala naye akamchukia na
kumwambia Tamali aondoke na akamchukia kwelikweli…..tafakari.
Hapa
kinachotendeka katika ulimwengu wa roho ni kependa umbo lakini my akionja hakuti
kile ambacho alikuwa anakifikiri.
Mfano mzuri
ni kwamba wanaume na wanawake wengi ambao wamedumu katika mapenzi hawaoani.
Mwanaume
akitembea na mwanamke na kutokukuta alichokitarajia, anasema hata kwa wenzake
kuwa ‘’demu mwenyewe mshamba na hana lolote’’ yote hiyo ni kuyachochea mapema
na kuvua.
Nitajuaje
kama ndiye?
Kimaandiko
unapomuomba Mungu, utawekewa rohoni kitu kinachoitwa mwongozo.
Utaona
unasukumwa na jambo la kuolewa kama kuku navyosumbuka kutafuta eneo la kutagia,
sawa na mtumishi wa Mungu anapotaka kufanya jambo la kiroho.
Jifunze
kumsikiliza Mungu, ondoa moyoni kufikiri kuwa huyo unayefikiri na kumweka
moyoni kama ni mwenyewe, huyo siyo. Achana naye maana roho ya mauti ipo juu
yako. Tubu.
MSIKILIZE
MUNGU ILI ASIKUJIBU SAWA SAWA NA VINYAGO ULIVYOWEKA MOYONI MWAKO NA KUJIINGIZA
POPOTE.
HEBU JIULIZE, MPAKA SASA UNA VINYAGO VINGAPI?
HEBU JIULIZE, MPAKA SASA UNA VINYAGO VINGAPI?
Hili ni somo
la sikio halisi, siku nyingine nitatoa mifano yangu halisi…..
Mungu awabariki na awasamehe wote
wenye toba.
Gordon Kalulunga
Information and Media
Consultant
P.O. Box 705,
Mbeya-Tanzania
Tel: 255 (0)754 440749
e-mail: kalulunga2006@gmail.com
WEB; www.kalulunga.blogspot.com
SODA INAVYOWEZA KUMFANYA MWANAUME KUWA TASA

Kwa mjimu
wa utafiti huo uliochapichwa kwenye Jarida la Epidemiology la Marekani,
wanaume wanaokunywa zaidi ya lita moja ya coca cola kwa siku
wanakabiliwa na hatari ya kuwa tasa. Wanaume
waliotumia kinywaji hicho walikuwa na upungufu wa aslimia 30 ya mbegu za
uzazi zilizohesabiwa, ikilinganishwa na wale ambao hawakutumia.
Wanaume
hao walionekana kuwa na matatizo ya uzazi zaidi kuliko wasiokunywa coca
cola.
MWALIMU WA MADRASAT AMPA MIMBA MWANAFUNZI, ATUPWA JELA MIAKA 7
M
|
walimu wa Chuo cha Madrasa kilichopo Chake Chake, Pemba, Said
Khamis Salum (31) ameanza kutumikia chuo cha mafunzo jela miaka 7 baada ya
kutiwa hatiani kwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 15 jina
(linahifadhiwa).
Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Bilali aliiambia Mahakama ya Chake Chake mbele ya hakimu, Khamis Ramadhan Abdalla kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo miezi mitatu iliyopita .
Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Bilali aliiambia Mahakama ya Chake Chake mbele ya hakimu, Khamis Ramadhan Abdalla kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo miezi mitatu iliyopita .
Bilali alisema mashahidi watano waliitwa mbele ya Mahakama na
kukiri kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Alisema baada ya uchunguzi wa vinasaba ( DNA), uliofanywa Tanzania Bara ulionesha kwamba kwa asilimia 96 mtuhumiwa ndiye aliyempa ujauzito mwanafunzi huyo.
Alisema baada ya uchunguzi wa vinasaba ( DNA), uliofanywa Tanzania Bara ulionesha kwamba kwa asilimia 96 mtuhumiwa ndiye aliyempa ujauzito mwanafunzi huyo.
Hakimu Abdalla alisema ameridhishwa na ushahidi wote, ikiwemo
ule wa kitaalamu wa vinasaba wa DNA, uliofanywa na wataalamu kutoka Tanzania
Bara, unaoonesha kwamba ni kweli mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Alisema mtuhumiwa atatumikia chuo cha mafunzo jela miaka saba,
na atakapotoka atalazimika kulipa fidia ya sh.milioni moja ikiwa ni fundisho
kwa wengine kuacha kufanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa wanafunzi wa vyuo
vya madrasa.
“Nimeridhishwa na mazingira ya makosa haya kwa mtuhumiwa na
kubaini kwamba ni kweli amempa ujauzito mwanafunzi wake wa chuo, kitendo
ambacho ni kinyume na sheria za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,” alisema
Adalla.
Mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea, alikana kosa hilo na
kusema anahisi kwamba alipitiwa na kurubuniwa na adui shetani, ambaye ndiye
aliyemshawishi kufanya hivyo.
Hivi karibuni, akizindua kampeni ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alikemea tabia ya baadhi ya walimu wa vyuo vya madrasa kuwafanyia ukatili wa kijinsia wanafunzi wao na wengine kuwapa ujauzito.
Hivi karibuni, akizindua kampeni ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alikemea tabia ya baadhi ya walimu wa vyuo vya madrasa kuwafanyia ukatili wa kijinsia wanafunzi wao na wengine kuwapa ujauzito.
Monday, 30 June 2014
KAMPENI YA mama Ye! NA RAIS JAKAYA KIKWETE, WANAVYOENDELEA KUHAKIKISHA MAMA NA WATOTO WACHANGA HAWAFI JWA UZEMBE
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
This message has been truncated
To Kalulunga2006@yahoo.com
Jun 28 at 11:19 AM
Dear Colleague,
Subscribe to:
Posts (Atom)